![]() |
| Kijana huyo mwenye umri wa miaka 15 anaendelea kupokea matibabu katika hospitali kuu ya Pathankot iliyoko katika jimbo la Punjab |
Polisi India wamesema kuwa kijana
mmoja amejipiga risasi kichwani kimakosa,akitafuta mbinu ya kujipiga
picha ya ''selfie'' ya kipekee akiwa na bastola ya babake.
Kijana
huyo mwenye umri wa miaka 15 anaendelea kupokea matibabu katika
hospitali kuu ya Pathankot iliyoko katika jimbo la Punjab Walioshuhudia wanasema kuwa alichukua bastola ya babake iliyoidhinishwa na serikali lakini kwa bahati mbaya akajipiga risasi kichwani akitaka kupiga selfie akiwa ameshika bastola kichwani.
![]() |
| Takriban nusu ya idadi ya vifo vya watu 27 vilivyotokea kote duniani mwaka wa 2015 kutokana na picha za ''selfie'' vimetokea nchini India. |
Takriban nusu ya idadi ya vifo vya watu 27 vilivyotokea kote duniani mwaka wa 2015 kutokana na picha za ''selfie'' vimetokea nchini India.



Post a Comment