By
Unknown
•
10:24:00
•
burudani
•
Mama mzazi wa legendary rapa Tupac Shakur amefariki dunia akiwa na
miaka 69,Kifo cha Afeni Shakur kimethibitishwa May 3 na taarifa
zilitolewa na Polisi wa Marin County mjini California.Ujumbe wa polisi
unasema Mama yake Tupac amefariki usiku wa May 2.
KRON wameripoti kuwa alipatwa na mshtuko wa moyo nyumbani kwake San
Francisco na kupelekwa hospitalini mida ya 9:45 p.m. nakutangazwa
amefariki mida ya 10:30 p.m.
Afeni Shakur alikuwa kwenye harakati za mwisho za kuchukua talaka kutoka kwa mume wake wa miaka 12 Gust Davis.
Afeni Shakur kwenye ujana wake alikuwa anatumia dawa za kulevya aina
ya Crack na alihusishwa na kundi la vijana la Black Panther.
SIMILAR ARTICLES
Post a Comment