Mtu wa karibu na familia ya The Carter ameliambia jarida la US Weekly
kuwa rapa Jay Z anarekodi nyimbo zitakazoeleza upande wake wa
kilichotokea kwenye ndoa yake na rnb staa Beyonce.
Queen Bey aliwashangaza mashabiki kwa video maalum iliyorushwa na
HBO pamoja na album ya Lemonade. Video hii ilielezea tetesi za muda
mrefu za usaliti wa mume wake kwa mashairi kama ya ” This is your final warning / You know I give you life / If you try this s‑‑t again / You gon’ lose your wife”.
Uvumi wa miaka miwili nyuma ulisema Jay Z na B walikuwa mbioni
kuachana kabisa baada ya tukio la ugomvi kwenye lifti. May 2014, TMZ
walivujisha video inayomuonesha mdogo wake Beyoncé, Solange Knowles,
akimshambulia Jay Z wakiwa kwenye lifti baada ya kuhudhuria hafla ya Met
Gala.
Home » burudani » Jay Z kufanya album atakayofunguka kuhusu tetesi za usaliti kama jibu kwa Beyonce na album yake yaLemonade
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


Post a Comment