Aliyekuwa Bondia wa uzani mzito duniani Lennox Lewis kushoto
Bondia wa zamani kutoka nchini
Uingereza Lenox Lewis amesema kuwa Amir Khan anaweza kumshangaza Saul
Canelo Alvarez siku ya Jumamosi iwapo atacheza mchezo wake.
Khan
mwenye umri wa miaka 29 ameruka mizani miwili ili kukabiliana na
mpinzani wake kutoka Mexico katika uzani wa kati mjini Las Vegas.
Katika onyesho la upimaji uzani wawili hao walikuwa na kilogramu 70.
Canelo Alvarez kushoto na Amir Khan kulia
''Khan anaweza kushinda iwapo hatamruhusu Canelo
kumfikia karibu.Khan ni bondia mzuri ,anatembea vizuri katika jukwaa na
kurusha ngumu nzuri,Lakini atahitaji kudhibiti matembezi yake dhidi ya
Canelo sio kukimbia bila mpango.Na pia lazima ujue kwamba sio yeye pekee
ataingia ulingoni na mkufunzi wake''.
Post a Comment