![]() |
| Maandamano ya Biafra |
Takriban watu saba waliuwawa siku ya
Jumatatu mashariki mwa mji wa Asaba, nchini Nigeria katika vita dhidi
ya watu wa jamii ya Biafra wanaotaka kujitenga na jeshi la taifa hilo
kulingana shirika la habari la Associated Press ripoti.
Zaidi ya watu milioni wameuawa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka wa 1967-1970, wakati jeshi lilipokuwa likipigana ili kuzuia mashariki mwa nchi hiyo kujitenga na kuunga jimbo linalojitengemea la Biafra.
Wanachama wa vuguvugu la jimbo la Biafra linalotaka kujitenga wameviambia vyombo vya habari kwamba idadi ya watu waliofariki ilikuwa juu ikilinganishwa na ile iliotolewa na maafisa wa polisi.
Raia wa Biafra na makundi mengine yaliyojitenga waliandamana siku ya jumatatu , siku ya ambayo walipata uhuru wao mwaka 1967


Post a Comment