Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania kutoka katika Kundi la Vituko Show,
Mohammed Abdallah ‘Kinyambe’ amefariki dunia Jumatano hii baada ya
kusumbuliwa kwa muda mrefu na uvimbe tumboni.
Taarifa za kifo chake zilianza kuzagaa jana katika mitandao ya
kijamii baada ya wasanii wa filamu kuanza kupost picha mbalimbali huku
wakiandika RIP Kinyambe.
Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii mmoja kati ya wasanii wanaounda
Chama Cha Wasanii Wachekeshaji Tanzania, Mkono Mkonole, amesema Kinyambe
amefariki jana akiwa mkoani Mbeya.
“Kinyambe alikuwa anasumbuliwa na uvimbe tumboni kwa muda mrefu, ila
jana ndo amefariki akiwa mkoani Mbeya, katika hospitali ya mkoa wa
Mbeya,” alisema Mkonole.
Kuhusu taratibu za mazishi, Mkonole amesema bado hawajapanga kwani taarifa za kifo chake wamezipokea jana usiku.
“Kusema kweli bado hatujapanga kuhusu mazishi, lakini sasa hivi
tunawasiliana na ndugu zake ili kujua taratibu za mazishi na zikamilika
tutaweka wazi,” alisema Mkono.
Kinyambe atakumbukwa kwa uwezo wake wa kuigiza, hasa hasa jinsi anavyoongea pamoja na mtindo wake wa pekee wa kugeuza macho.
Baada ya taarifa hizo, wasanii mbalimbali wa filamu na muziki
walishare ya moyoni jinsi walivyozipokea taarifa hizo za kusikitisha.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


Post a Comment