Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo imetangaza kuwachukulia
hatua kali za kisheria wasanii ambao watakiuka agizo la kufanya video za
muziki na kuzitoa bila kukaguliwa na Bodi ya Filamu ili zikaguliwe.
Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa wizara hiyo, Zawadi Msalla, amewaonya wasanii kuendelea kufanya kazi zao za muziki bila kufuata taratibu.
Zawadi Msalla anasema “Taratibu
zinaeleza wazi, kwamba kabla ya kushoot video yako unatakiwa upeleke
script ikaguliwe kwanza na baada ya hapo utapewa ruhusa ya kuendelea,”
“Sasa hivi tutakuwa wakali kweli hili, hili ni swala la kisheria
taratibu ziko hivyo, kwa hiyo nikufuata taratibu tu,” aliongeza.
Kwa upande wa Mwanasheria wa Wizara ya Habari amesema msanii
kuendesha kazi bila ya kuzingatia sheria ni kosa huku akiwataka wasanii
kupeleka kazi zao Bodi ya Filamu kukaguliwa kabla ya kutoka.
Mwanasheria >>“Snura
hajajisajili, ametoa kazi bila ya kupata kibali pamoja na kuitoa nyimbo
bila ya kuipeleka sehemu husika kwa ajili ya kuifanyia ukaguzi ili
kuithibitisha kama inafaa,”
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


Post a Comment