Baada ya kupondwa sana kwa rapa Desiigner kufanana sauti na Future
kwenye wimbo wake wa PANDA ambao ulishika namba moja kwenye chati za
billboard producer mkongwe Jermaine Dupri naye alisema kuwa mdundo wa
PANDA umeibiwa na kukopiwa moja kwa moja kutoka kwenye mdundo wa Future
wa “Fuck Up Some Commas.”
Producer wa Panda kutoka Uingereza Menace amefunguka juu ya tuhuma za
kukopi biti nakusema “Timu yangu imesikiliza na kugundua kuwa hakuna
chochote kilichofanana kati ya kazi hizi mbili,nimetumia vinanda zaidi
na kwenye wimbo wa Future vinanda vichache sana,nimetengeneza biti hii
mwaka 2014,nimetengeneza wimbo huu kutokana na style ya Grime kutoka
Uingereza”.
Mpaka sasa Menace anasema amewatumia biti wasanii Lil Wayne, French Montana, Ty Dolla $ign, T-Pain na Vado.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


Post a Comment