Kenya inakabiliwa na changamoto upya
kuhusiana na sheria ya kukabili matumizi ya madawa ya kututumua misuli
miongoni mwa wanariadha wake.
Kamati hiyo inapendekeza kuwa hatua ichukuliwe dhidi ya Kenya kwa kujumuisha vipengee fulani ambavyo vinakinzana na kanuni za WADA.
BBC imebaini kuwa halmashauri kuu ya WADA itakubali mapendekezo hayo katika mkutano wao mkuu baadaye leo mjini Montreal Canada.
Iwapo hilo litatekelezwa basi itakuwa wajibu wa kamati ya olimpiki duniani IOC kuipiga marufuku Kenya kutoshiriki mashindano yake hadi pale itakapotekeleza masharti iliyowekewa.
WADA ilikuwa imeipa Kenya makataa mapya ya hadi Mei 2 kuidhinisha sheria hiyo la sivyo ikabiliwe na hatari ya kuadhibiwa.
Takriban wanariadha 40 wameadhibiwa na shirika la riadha duniani (IAAF) kwa kupatikana wakiwa wametumia dawa hizo tangu mwaka 2012.
Bingwa mtetezi wa mbio za Boston marathon na Chicago pia ni miongoni mwa walioadhibiwa.
WADA ilikuwa imetoa masharti makali ya kudhibiti matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwili, pamoja na kutolewa kwa ufadhili wa kila mwaka wa $50,000 milioni kwa idara ya kukabiliana na tatizo hilo.
Tatizo la dawa zilizoharamishwa Kenya
Kufikia Januari 2016, wanariadha 18 wa Kenya walikuwa wanatumikia marufuku
Wanariadha hao 18 walikuwa wanatumikia marufuku ya jumla ya miaka 55
Maarufu zaidi ni Rita Jeptoo, mshindi wa marathon za Boston na Chicago Lilian Moraa Mariita anatumikia marufuku ndefu zaidi – miaka minane


Post a Comment