50 Cent amekamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha polisi huko Saint Kitts kwenye visiwa vya Caribbean kwa kosa la kutukana akiwa jukwanii kwenye show.
Kwa mujibu wa TMZ 50 Cent alisema neno “motherf**kin’” akiwa anaimba wimbo wa “P.I.M.P.” mbele ya mashabiki 40,000 waliohudhuria na matusi hayo yalirekodiw kwenye simu na watu walioko kwenye show.
Polisi walimkamata 50 Cent kwa kutumia lugha chafu kwenye umati wa watu na atabidi afikishwe mahakamani na kulipa faini.
Mwaka 2013, DMX alikamatwa hapo hapo kwa kutumia matusi jukwaani na alilipishwa faini.


Post a Comment