Rapa Kanye West ametoa video ya wimbo wake wa “Famous” kutoka kwenye album yake ya saba ya “The Life of Pablo” na kila mtu anaizungumzia video hii.
Video inaonyesha mwili wa Kanye na mke wake Kim Kardashian wakiwa wamelala watupu kwenye kitanda kimoja pamoja na mastaa tofauti.
Mastaa hawa ni pamoja na George W. Bush, Anna Wintour, Donald Trump, Rihanna, Chris Brown,Ray J, Amber Rose, Caitlyn Jenner, Bill Cosby na Taylor Swift.
Ukiangalia kwa karibu bado huwezi kujua mwili upi wa msanii yupi ni wa kweli na upi umetengenezwa tu.
Vanity Fair imeripoti kuwa video hii imechukua miezi mitatu kutengeneza na kupitishwa kwenye mifumo zaidi ya minne mpaka Kanye kupata kitu alichotaka.
Shabiki mmoja kwenye mtandao wa twitter anasema picha hii imetokana na mchoro waVincent Desiderio uliopewa jina “Sleep” unaonyesha watu 12 wakilala kwenye kitanda kimoja.



Post a Comment