Latest in Tech

Meli 14 za kijeshi hazijulikani zilipo, Uturuki

Meli 14 za kijeshi hazijulikani zilipo, Uturuki
Manahodha wa meli kadhaa za Uturuki wameripotiwa kushindwa kuwasiliana na ofisi yao kuu wiki moja baada ya kufeli kwa jaribio la kutaka kuipendua serikali ya Rais Recep Tayyip Erdogan.
Inasemekana makamanda wa meli hizo ni miongoni mwa maafisa waliohusika katika jaribio hilo la kutaka kuipindua serikali na sasa huenda wameamua kutoroka.
Pia kiongozi wa majeshi hao wanamaji Admiral Veysel Kosele bado hajulikano alipo.
Image copyrightGETTY
Image captionPia kiongozi wa majeshi hao wanamaji Admiral Veysel Kosele bado hajulikano alipo.
Serikali ya Uturuki inasema ingali inawasaka maafisa wengineo wanaotuhumiwa kuhusika na jaribio hilo la mapinduzi -- Tayari karibu maafisa elfu 18 kutoka jeshini, idara ya polisi na hata majaji wameshasimamishwa kazi au kutiwa nguvuni.
Zaidi ya hayo utawala wa rais Erdogan unasema unatafakhari namna ya kurudisha tena hukumu ya kifo kwa watakaopatwa na hatia ya makosa makubwa kama vile uhaini.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes