Latest in Tech

TOPIC: Faida za Bilinganya, Vitunguu na Nyanya Mwilini mwako


· Bilinganya huzuia ugonjwa wa moyo, saratani, kiharusi
· Vitunguu maji , Saum kusaidia msukumo wa damu, hupunguza mabujabuja ya damu (blood clotting).
· Nyanya hupunguza hatari ya moyo, saratani

Na Abdallah Bendada
Mabilinganya (eggplants)

Yana kiwango cha juu cha nyuzinyuzi, yana kiwango cha chini cha mafuta na yana wingi wa virutubisho kama vile vitamini A na C, kundi la vitamini B (niacin), na asidi jani na madini ya chuma, kalisiamu, magnesiamu na potasiamu.

Ngozi ya bilinganya ina wingi wa virutubisho vya kuzuia magonjwa ya moyo na saratani, na ina virutubisho vingine vinavyoweza kusaidia kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na kiharusi. Aidha ngozi ya bilinganya inaambatana na miseto iitwayo terpenes ambayo huweza kusaidia kupunguza lehemu.

Vitunguu Saumu (garlic)
kwa karne nyingi,vimegundulika kuwa na manufaa ya kiafya. Utafiti wa hivi karibuni kabisa umefichua faida ya ndani ya kiafya ya kitunguu swaumu itokanayo na mseto uitwao allicin uliomo katika kitunguu hicho ambao ndio unaokifanya kiwe na ladha na harufu kali ya kunukia.


Wanasayansi waligundua kuwa mseto wa allicin huoza ili kutengeneza sulfenic acid, ambacho ni ki-kemikali kinachochachamaa kupambana na chembechembe za maradhi zinazoweza kusababisha saratani. Vitunguu maji na vitunguu saumu vina miseto ya chumvichumi za kioganiki ambayo hujitokeza kusaidia msukumo wa damu na kupunguza mabujabuja ya damu (blood clotting).


Nyanya

Hili ni tunda mashuhuri na lenye virutubisho ambalo kwa kawaida hutumika kama mbogamboga. Kwa wastani, watu hula takribani kilo 8 za nyanya kwa mwaka.

Nyanya zina aina mbalimbali za viasili vya kurutubisha na visivyorutubisha vinavyohusiana na faida kadha wa kadha za kiafya. Hii inajumuisha lycopene, vitamini C, A na K, potasiamu, na nyuzinyuzi.

Nyanya moja yenye ukubwa wa wastani inaweza kutoa takribani nusu ya kiasi cha kila siku cha vitamini C anachohitajika kupata mtu. Viasili mbalimbali vya nyanya vinasadikika kufanya kazi pamoja kuleta manufaa ya kiafya.

Hii ni pamoja na kusaidia kujenga afya ya meno, afya ya mifupa, afya ya ngozi, afya ya nywele, kupunguza shinikizo la damu (PB) na kupunguza viwango vya lehemu pamoja na kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na saratani.

Baadhi ya vionjo vya nyanya kama vile lycopene hufyonzwa kwa wepesi mwilini pale nyanya zinapochemshwa, iwe kwa kuzipika au kuzichemsha.

Sasa huenda tunazijua faida za kula lishe kamili ya kuleta afya ikiwa ni pamoja na kula matunda na mbogamboga. Lakini wasichokijua watu wengi ni kwamba juisi ya mbogamboga ndiyo inayosaidia kudumisha urari (pH) muhimu wa haidrojeni ya mwili.

pH ina maana ya nguvu ya haidrojeni katika mizani ya kupimia hali-asidi ya vitu mwilini. Ili mwili ufanye kazi vizuri na kuweza kuendelea kuishi, lazima uwe na vikemikali vinavyolipuka na vitu vya asidi ili kutengeneza chumvi na kutoa umajimaji wenye nguvu ya haidrojeni (ya baina ya 7 na 7.5) na uwe na kipimo cha haidrojeni chenye urari kamili kwa sababu saba:

1. Kuulinda mwili dhidi ya uharibifu utokanao na chembechembe za maradhi na kuukinga na uzee wa kabla ya wakati.
2. Kuusaidia mwili kudumisha viwango vya lehemu vyenye kuleta afya bora.
3. Kuweka msukumo wa damu katika kiwango bora cha afya.
4. Kuweka katika hali ya kawaida kikemikali cha kusawazisha sukari ya damu (insulin) na kuzuia ongezeko la uzito wa mwili linaloweza kuhatarisha afya.
5. Kuuwezesha moyo kufanya kazi vizuri.
6. Kuongeza uzalishaji wa nishati
7. Kudumisha mfumo wa kinga ya mwili, mfumo wa umeng’enyaji, kudumisha afya ya viungo vya mwili na mifupa

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes