Latest in Tech

Ciara ataja hasara aliyopata baada ya kudhalilishwa na Ex wake Future.

Rnb staa Ciara ambaye alikuwa mchumba wa rapa Future ametaja kiasi cha pesa alichopoteza baada ya udhalilishaji aliofanyiwa na Ex wake Future.
Ciara anasema maneno ya Future kwenye twitter kuhusu yeye yaliwaogopesha na kuwakimbiza wasajili wa kampuni kubwa ya vipodozi waliokuwa tayari kulipa zaidi ya dola Laki Tano $500,000.
Ciara alifungua kesi hio mwanzoni mwa  mwaka huu baada ya Future kumuita “bitch” with “control problems” kwenye mtandao wa twitter.
Ciara analalamika kuwa maneno hayo yamefanya watu wanaotaka kufanya nae kazi wakimbie wakidhani yeye ni mtu anaye penda Kuendesha watu, muongo, muharibifu, hana maana, Shetani na msiri sana.
Fahamu baada Ciara kuachana na Future, ameolewa na staa wa NFL Russell Wilson.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes