Kwenye interview kuhusu kutaka kugombea urais rapa Kanye West ametoa maelezo ya mtazamo wake juu ya kuwa rais na mabadiliko anayotaka kufanya.
Kanye West anasema ” Tuko kimya kuhusu watoto 500 kupoteza maisha yao mjini Chicago, polisi wamepiga watu risasi mara saba kwa mwezi wa saba tu, tuko kimya wakati watu kwenye nchi zingine wanapoteza maisha kama vile sisi hatupo duniani au hatuoni, Nikiongelea swala la Urais sina mambo ya SIASA mimi, ni taka tuwe na ubinadamu zaidi, ukweli duniani, kama naweza kufanya chochote kubadilisha maisha ya watu nitafanya“.


Post a Comment