Latest in Tech

MICHEZO

SIASA

VIDEOS

Latest Updates

Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

UFC 202: Conor McGregor amcharaza Nate Diaz, pambano latawaliwa na damu (Picha)

11:41:00
Bondia Conor McGregor ameibuka mshindi dhidi ya Nate Diaz kwenye pambano la UFC 202 lililofanyika wikiendi hii.
377405E000000578-3751207-image-a-3_1471757130370
Ushindi huo ni kisasi cha McGregor dhidi ya Diaz aliyemshinda kwenye pambano lao lililopita.
Mahasimu hao walikumbatiana baada ya pambano kuisha na kushuhudia Diaz akienda chini mara tatu.
37740FA900000578-3751207-image-m-132_1471755171312
Diaz alionekana kuumizwa zaidi kwenye pambano hilo huku uso wake ukijaa damu. Diaz ametaka pambano la tatu.
Tazama picha zaidi:
3773F89500000578-3751207-image-m-66_1471752266117
37740AE100000578-3751207-image-m-129_1471755119674
37740FBD00000578-3751207-image-m-128_1471755105138
37741A1A00000578-3751207-image-a-6_1471757397940
377414EB00000578-3751207-image-a-34_1471758175828
377417FB00000578-3751207-image-a-31_1471758006073
3774000C00000578-3751207-image-m-74_1471752534111
3774059C00000578-3751207-image-m-83_1471753561111
3774109D00000578-3751207-image-a-12_1471757580572
3774156C00000578-3751207-image-a-15_1471757712379

POGBA asaini mkataba wa miaka mitano Man U

01:31:00
Paul Pogba amesema kuwa ni muda muafaka kurejea Old Trafford baada ya uhamisho wake wa Paundi 89 ulioweka rekodi ya dunia kwenda Manchester United.
Kiungo huyo mwenye miaka 23 anarejea tena klabuni hapo baada ya miaka minne alipoelekea Juventus kwa ada ya uhamisho wa pauni 1.5 milioni mwaka 2012.
Pogba, ambaye amesaini mkataba wa miaka mitano ameongeza kuwa ''hii ni klabu sahihi kwangu kupata mafanikio ninayoyahitaji.''
Meneja wa Man U Jose Mourinho amesema Pogba atakuwa muhimili mkubwa wa klabu hiyo kwa kipindi kirefu kijacho.
United itailipa Juventus ambao ni mabingwa wa Italia Euro 105 milioni sambamba na Euro 5 milioni ikiwa hii ikitegemea kiwango chake kitakavyokuwa.
Uhamisho uliokuwa wa gharama na kushikilia rekodi ni wa Gareth Bale aliyetokea Spurs kwenda Real Madrid ukiwa ni Paundi 85.
pogba ndani ya jiji la manchester
Pogba aliyeisaidia Ufaransa wenyeji wa michuano ya Euro 2016 kufika fainali ameshinda taji la Serie A katika miaka yote minne ndani ya klabu yake.

Bastian Schweinsteiger atangaza kustaafu soka la kimataifa

05:31:00
Mchezaji na kiungo wa Manchester United, Bastian Schweinsteiger, ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani, ikiwa ni majuma kadhaa baada ya timu hiyo kushindwa kufikia malengo ya kutwaa ubingwa wa barani Ulaya.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31, alikuwa sehemu ya mafanikio yaliyopatikana wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014, ambapo Ujerumani walitwaa ubingwa wa fainali hizo katika ardhi ya Brazil kwa kuifunga bao moja timu ya taifa ya Argentina.
Schweinsteiger, ametangaza kustaafu soka la kimataifa huku akiacha kumbu kumbu ya kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani katika michezo 120 sambamba na kufunga mabao 24.
“Katika michezo 120 niliyocheza nikiwa na timu yangu ya taifa, sina budi kujivunia kwa mafanikio niliyoyapata na ninaamini kipindi hiki ni sahihi kwangu kutangaza kuachana na timu hiyo, ili kupisha wachezaji wengine,”Imeeleza taarifa ya Schweinsteiger.

Gonzalo anunuliwa kwa pauni milioni 75

00:54:00
Juventus wamemnunua mshambuliaji wa Agentina Gonzalo Higuain kutoka Timu ya Napoli kwa pauni milioni 75.5
Mchezaji huyo mwenye miaka 28 amesaini mkataba wa miaka mitano baada ya Juventus kukubali kutoa kitita hicho kinachokaribia Euro milioni 90 ambazo watazilipa kwa awamu.
Malipo hayo ya Mzaliwa wa Ufaransa Higuain aliyeanzia uchezaji wake wa kulipwa katika timu ya River Plate ya Argentina yanachukua nafasi ya tatu kwa ukubwa baada ya yale yaliyolipwa na Real Madrid walipomnunua Cristiano Ronaldo kwa Pauni milioni 80 na Gareth Bale kwa Pauni milioni 85.

VIDEO: Cristiano Ronaldo akiwa kwenye show ya Jennifer Lopez Las Vegas

09:00:00
Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo ambaye hivi sasa yupo likizo baada ya michuano ya Euro 2016, July 24 2016 alioneka akiwa Las Vegas, Marekani kwenye show ya Jennifer Lopez.
maxresdefault
Ronaldo ambaye wiki kadhaa alikuwa katika fukwe za Ibiza, Hispania na familia yake akiwa katika boti ya kifahari, July 24 ameonekana akiwa na rafiki yake waki furahia katika show ya J.Lo kwa sasa Ronaldo bado anauguza jeraha lake la goti.
Video Ronaldo akiwa katika show ya J.Lo huko Las Vegas, Marekani


Guardiola ''nitasalimiana na Mourinho kwa mkono''

08:54:00
Meneja mpya wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola, amesema hatakuwa na tatizo lolote kumsalamia kwa mkono meneja wa Man U Jose Mourinho, wakat wa mechi kati ya vilabu hivyo mjini Beijing.
mourinho-guardiola1
Mechi hiyo itakuwa ya pili kati yao tangu wote waache kufunza vilabu vya Barcelona na Real Madrid mwaka 2012.
Wote wamekana tofauti zoa na Guardiola anasme kuwa atamsalamia kwa mkono kama njia ya urafiki.
Wakati Mourinho naye aliulizwa kuhusu suala hilo, pia alisema kuwa atamsalamia Guardiola kwa mkono.
“Nilifanya kazi naye kwa miaka mitatu huko Barcelona, Tumesimamia tofauti, uhusiano kati yetu ni wa kawaida, alisema Mourinho.

Kolo Toure amesajiliwa rasmi na klabu ya Celtic ya Scotland

08:52:00
Beki wa kati wa kimataifa wa Ivory Coast aliyewahi kuvichezea vilabu vya Arsenal, Man City na Liverpool Kolo Toure, mwenye umri wa miaka 35, ametangazwa kusajiliwa na klabu ya Celtic ya Scotland kwa mkataba wa mwaka mmoja, hiyo itakuwa ni mara ya pili kwa Kolo Toure kufundishwa tena na kocha Brendan Rodgers ambaye amewahi kumfundisha katika kikosi cha Liverpool.

Aliyefanya jaribio la kuiba mwenge wa Olimpiki Brazil atiwa mbaroni

08:43:00
Polisi nchini Brazil, wamemtia mbaroni mtu mmoja ambaye alijaribu kuiba mwenge wa Olimpiki, ilipokuwa ikipitishwa katika jimbo la Sao Paulo.
t04_20908853
Video kuhusiana na tukio hilo, inamuonyesha mtu huyo akipigwa mieleka na walinda usalama, baada ya kuingia katika msafara wa watu na kuelekea moja kwa moja hadi kwa mtu aliyekuwa na mwenge huyo akiwa na nia ya kumpokonya.
Mtu huyu alinaswa na kuchukuliwa, huku mbio za mamani za mwenge huo zikiendelea muda mfupi baadaye.
Mwenge huo unatazamiwa kufika mjini Rio de Janeiro tarehe 4 mwezi ujao, kabla ya kuanza rasmi kwa mashindano ya Olimpiki.
 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes