Mkutano wa mawaziri wa fedha wa mataifa ya G20, umemalizika nchini China, huku onyo likitolewa kuwa, kura ya maoni iliyoifanya Uingereza kujiondoa ndani ya muungano wa mataifa ya Bara Ulaya, imesababisha hatari kubwa zaidi na kuyumbisha uchumi wa Dunia.
Mkutano huo wa G20 umesema kwamba kuna hatari kubwa kuwa, mazungumzo kuhusiana na hatua hiyo ya Uingereza yakaibua uchungu mwingi.
Lakini viongozi hao wakasema kuwa EU imejiandaa ipasavyo kushughulikia tatizo hilo huku wakisema kuwa wana matumaini kubwa kuwa Uingereza sharti iendelee kuwa mshirikamkubwa wa EU.
Mataifa mengi barani Afrika yameathirika pakubwa na baa la njaa.
Ima ni kutokana na mabadiliko ya hali ya anga , ukosefu wa pembejeo za kilimo, ama hata ukosefu wa nguvu kazi ya kuendeleza kilimo.
Kutokana na uhaba wa chakula wa mara kwa mara nchini Nigeria , Mhandisi mmoja amebuni na kuzindua trekta iliyoundwa nchini Nigeria.
Mhandisi Timothy Addigi Terfa ameiambia BBC kuwa alizindua trekta hiyo ya bei nafuu kwa sababu ya upungufu wa mashine hiyo barani Afrika na athari yake kwa kilimo nchini Nigeria.
Aidha mhandisi huyo alisema bei ya trekta barani Afrika inakohitajika mno ni ghali mno.
IJODO
Kulingana naye upungufu huo umesababisha wakulima wengi kuendelea kutumia mikono yao kuendeleza kilimo shambani na hivyo kuathiri pakubwa kiwango cha chakula kinachozalishwa.
Image captionKila trekta aliyounda katika karakana yake itauzwa kwa takriban dola elfu 3,500.
Hilo kwa maoni yake linachangia pakubwa uhaba wa chakula nchini humo.
Kila trekta aliyounda katika karakana yake itauzwa kwa takriban dola elfu 3,500.
Trekta hizo za ''made in nigeria'' zinaitwa IJODO.
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kuwa shirika la ndege la Tanzania litarejea angani ''kabla ya mwisho wa mwezi Septemba Mwaka huu 2016''.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya ikulu ya Tanzania bw Gerson Msigwa
''Dkt. Magufuli amesema serikali yake imechukua hatua madhubuti za kulifufua shirika la ndege la Taifa.
Tayari mipango imefanywa kuhakikisha ndege mbili aina Bombadier Q400 zinanunuliwa na zitatua hapa nchini kabla ya mwisho wa mwezi Septemba Mwaka huu 2016.'' taarifa hiyo inaeleza.
Tamko hilo ni ishara nzuri kwa sekta ya uchukuzi nchini Tanzania na vilevile kanda nzima ya Afrika Mashariki ambayo imekuwa ikikabiliwa na gharama za juu za usafiri kutoka kwa mashirika ya kigeni.
BIASHARA NA RWANDA
Wakati huohuo rais Magufuli aliueleza ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Rwanda kuwa China imeonesha nia ya kushirikiana na Tanzania kujenga reli ya kisasa yaani “Standard Gauge” kwa nia ya kurahisisha uchukuzi wa mizigo kutoka bandari ya Dar es salaam kwa manufaa ya wafanyabiashara.
Image captionMarais Paul Kagame na mwenyeji wake John Magufuli
''Tanzania imeamua kuipatia Rwanda eneo la kujenga bandari kavu kwa ajili ya mizigo ya wafanyabiashara wake na pia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) itafungua ofisi mjini Kigali nchini Rwanda ikiwa ni juhudi za kurahisisha na kuongeza biashara kati ya nchi hizi mbili.''
Juhudi hizo bw Magufuli anasema ni kuwahakikishia wafanyabiashara wa Rwanda kuwa bandari ya Dar es salaam ni salama kwao kupitisha mizigo na ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania inaendelea kuchukua hatua za kuimarisha bandari hiyo na kurahisisha biashara kati ya nchi hizi mbili.
Kwa upande wake rais Paul Kagame wa Rwanda alitoa wito kwa ''Tanzania na Rwanda pamoja na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana na sekta binafsi katika kutumia fursa nyingi za kibiashara zilizopo baina yake na kuwaletea manufaa wananchi''.
Bei ya mafuta imepanda hadi zaidi ya
dola 50 kwa pipa kwa mara ya kwanza kabisa mwaka huu mwaka 2016 wakati
uzalishaji wa chini na kuongozeka kwa mahitaji ya mafuta vikiendelea
kuchangia kupanda kwa bei.
Kupanda kwa bei ya mafuta kunafuatia
takwimu za Marekani zinazoonyesha kushuka kwa uzalishaji hasusan
kutokana na moto nchini Canada. Uzalishaji wa mafuta yasiyosafishwa nchini Marekani
ulishuka kwa pipa milioni 4.2 hadi pipa milioni 537.1 kwa wiki kwa
mujibu wa idara ya nishati nchini humo..
Canada ndiye muuzaji
mkubwa zaidi wa mafuta kwa Marekani na moto wa msituni katika mikoa
iliyo magharibi, ulisababisha kupungua kwa karibu mapipa milioni moja
kwa siku.
Mazungumzo ya hivi majuzi kati ya nchi za Opec na Urusi kuhusu kupunguza uzalishaji wa mafuta yamechangia kupanda kwa bei.
Baada ya kutumia gharama kubwa mwaka 2014 kuinunua Nokia, Microsoft imeamua kuiuza kwa kampuni ya Foxconn kwa dola milioni 350.
Kwenye dili hiyo kampuni tawi la Foxconn, FIH Mobile Ltd. Itakichukua
kiwanda cha simu cha Microsoft kilichopo Vietnam. Microsoft pia
inaigawa brand ya Nokia na mambo mengine.
Hiyo haimaanishi kuwa Microsoft inajiondoa kabisa kwenye utengenezaji wa simu – itaacha tu kutengeneza vifaa vya Nokia.
Katika maelezo yake, Microsoft inasema itaendelea kutengeneza
Windows 10 Mobile na kusupport simu kama Lumia 650, Lumia 950 na Lumia
950 XL, na simu za kampuni rafiki ya OEM za Acer, Alcatel, HP, Trinity
na VAIO.
Hivi karibuni Microsoft ilipunguza wafanyakazi 8,000 kutoka kwenye
idara yake ya simu na kuziachia dola bilioni 7.6 ilizozitumia kwenye
Nokia.
Leo kampuni kubwa ya simu ya Nokia imetangaza rasmi kuanza
kutengeneza smart phone za kisasa kutoka kwenye kampuni yao
itakayotengeneza simu hizo ya Global HMD. Kampuni hii itawasaidia Nokia
kuweza kutengeneza na kuuza simu za Android na tablets.
Kumbuka kuwa kampuni ya Microsoft ndio ina haki za kuuza na
kutengeneza Nokia handset toka mwaka 2014, na kwa sasa inauza haki hizo
kwa kampuni ya Foxconn’s FIH kwa dola milioni $350 million.
Hii imetajwa kuwa gari ya bei rahisi zaidi nchini China, gari hii
inaitwa Jiangnan TT inatengenezwa na kampuni ya Jiangnan Auto, bei yani
ni 20,800 yuan na punguzo lake ni mpaka 5,000 yuan. Kwa mahesabu ya
haraka haraka ni kama dola za kimarekani $2,415 ambayo ni milioni tano
za Bongo.
Cylinder tatu, mafuta ni 0.8 liter ha 36 horsepower, speed ya 120
kilometers per hour (75 miles). Gearbox is a four-speed manual.
Ukame umesababisha ukosefu wa chakula kwenye nchi za kusini mwa Afrika
Shirika la kimataifa la msalaba
mwekundu na chama cha msalaba mwekund wametoa ombi la dola milioni 110
kusaidia nchini za kusini mwa Afrika zilizoathirika na ukame.
Takriban watu milioni 31.6 katika eneo hilo hawana chakula cha kuwatosha kutokana na ukosefu wa mvua na uhaba wa maji.
Ombi
hilo linatolewa kabla ya kufanyika mkutano mkuu wa umoja waimataifa,
unatarajiwa kuangazia hitaji la kuchukua hatua, kulinda jamii kutokana
na mabadiliko ya hali ya hewa.