Timu ya Taifa ya Tanzania inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa Kenya Mei 29, jijini Nairobi.
TFF kwa kushirkiana na FKF zimekubaliana kuwepo kwa mchezo huo wa kirafiki, utakotumika kama sehemu za maandalizi kwa timu zote kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 mwezi Juni.
Kikosi cha Taifa Stars kinachonolewa na kocha mkuu, Charles Boniface Mkwasa kinatarajiwa kuingia kambini mwezi Mei, mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Vodacom (VPL) kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuwakabili Misri mwezi Juni, 2016.
Post a Comment