![]() |
Uganda kupitishia mafuta yake Tanzania |
Uganda imeamua kujenga bomba la mafuta yake kupitia Tanzania na wala sio Kenya.
![]() |
Uganda imeelezea wasiwasi wa mabomba ya mafuta kushambuliwa na wanamgambo wa Alshabab |
Uganda imeelezea wasiwasi wa mabomba ya mafuta kushambuliwa na wanamgambo wa Alshabab kwani bomba hilo la kupitia Kenya linatazamiwa kutumia bandari ya Lamu.
Uganda ilitangaza uamuzi wake katika kongamano la viongozi wa muungano wa Afrika Mashariki uliokuwa mji mkuu wa Kampala.
Bomba hilo la mafuta litakwenda kilomita 1,400km kuanzia Hoima, hadi kwenye bandari ya Tanga.
Mradi huo utagharimu takriban dola bilioni $4 za Marekani.
Aidha ujenzi huo unatarajiwa kutoa nafasi za kazi 15,000 kwa vijana ambao wanatatizika sana na uhaba wa ajira.
Kampuni ya mfuta ya Ufaransa Total, ile ya China CNOOC na ile ya Uingereza Tullow ndizo zinazomiliki leseni ya kuchimba na kusafisha mafuta nchini Uganda.
Kenya sasa imeamua kujenga bomba lake kufuatia uamuzi huo wa Uganda.
Post a Comment