Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza rasmi
kumfungia msanii wa bongo fleva Snura kujihusisha na masuala ya sanaa.
Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Zawadi Msalla ameongea na waandishi wa habari na kuthibitisha
taarifa hizi.
Wimbo huu wa Chura umefungiwa kupata muda wa hewani kwenye redio na
TV nchini. Taarifa hiyo imetolewa na wizara hiyo kwenye mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wake wa mikutano wizarani
hapo Dar es salaam.
Uamuzi wa kumfungia umekuja kutokana msanii huyo kutojisajili kwenye Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


Post a Comment