Latest in Tech

DIRECTOR HANSCANA AIKACHA WANENE

Muongozaji wa video Tanzania,Hascana amefunguka kuhusu tetesi zilizoenea kwamba amefukuzwa kazi kwenye studio za Wanene entertainment ambazo zilikuwa zinamsimamia katika kazi zake za uongozaji wa video.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo,Hascana amesema kuwa yeye hajafukuzwa na studio hizo bali yeye ndiye amevunja mkataba wa kufanya kazi na studio hizo na kuamua kujitegemea baada ya kuona tayari ameshafanya studio hizo zijulikane ambapo ndio ilikuwa kazi yake kubwa.
Wanene hawawezi kunifukuza kazi” alisema Hanscana, “ni kweli kwa sasa sifanyi kazi na Wanene,jukumu langu likuwa ni kufanya watu waifahamu wanene,kwa kuwa tayari imeshafahamika,jukumu langu nimeshakamilisha” aliongeza Hascana na kusema,”Nimeamua wakati huu kusimama Hascana kama Hascana lakini hatuna ugomvi wowote” na kuongeza kuwa mkataba wake ulitakiwa uishe mwakani lakini ameusitissha baada ya kuona studio hizo zina uwezo wa kusiamama peke yake.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes