Latest in Tech

MPANGILIO WA SAYARI NA MAGIMBA KATIKA JUA

Mfumo wa jua na sayari zake


Jua letu na sayari zake.
Mfumo wa jua na sayari zake ni utaratibu wa jua letu na sayari au sayari kibete zinazolizunguka pamoja na miezi yao, asteroidi, meteoridi, kometi na vumbi ya angani, vyote vikishikwa na mvutano wa jua.
Utaalamu kuhusu mfumo wa jua hujadiliwa katika fani ya astronomia.
Kwa kawaida huhesabiwa sayari 9 zinazozunguka jua. Lakini miaka ya nyuma magimba makubwa yamegunduliwa angani ambayo bado hayajakubaliwa kama yahesabiwe kuwa sayari au aina ya asteoridi.
Orodha inayofuata bado inahitaji kuangaliwa kwa sababu kuna tofauti kati ya kamusi na vitabu mbalimbali jinsi ya kutaja sayari fulani.

Sayari za jua letu


Sayari mbili kubwa za buluu karibu na sayari mbili kubwa kabisa zilizoundwa hasa na gesi, pamoja na sayari ndogo kama dunia yetu.[1]
Sayari katika mfumo wa jua ni zifuatazo:
Namba zote zinazotaja sifa mbalimbali za sayari zinaonyesha kipimo kulingana na tabia za dunia yetu kuwa "1". Kuhusu majina ya sayari kadhaa kuna mchanganyiko katika kamusi na vitabu. Pale ambako jina au umbo tofauti la jina ni la kawaida linaonyeshwa katika mabano kama (jina). Majina yanayotumiwa katika vitabu kadhaa, hasa vya shule za msingi, bila kuwa na uhakika yanaonyeshwa katika mabano ya italiki pamoja na alama ya swali kama (? jina). [2]
* Utaridi ni jina la sayari ya kwanza kutokana na lugha ya Kiarabu na pia katika mapokeo ya Kiswahili tangu kale. Vitabu vingine hutumia neno "Zebaki" ambalo pia lina asili ya Kiarabu likimaanisha metali mojawapo; inaonekana limepatikana kama tafsiri ya jina la Kiingereza la sayari ya kwanza "Mercury" bila kujua historia ya majina ya sayari sita ya kwanza yaliyoingia katika Kiswahili kutoka lugha ya Kiarabu. [3]
** Zuhura - Ng'andu ni sayari ambalo kwa Kiswahili lina jina la Kibantu pamoja na jina lenye asili ya Kiarabu
*** Tazama makala ya Dunia kwa ajili ya namba halisi. Neno "ardhi" hutumika na waandishi kadhaa badala ya "dunia" wakitaka kutaja sayari ya tatu.
**** Tangu mwaka 2006 Pluto imeingizwa katika kundi la "sayari kibete" Katika vitabu vya shule ya msingi inatajwa mara nyingi kwa jina Utaridi - ambayo haiwezekani maana Pluto haikujulikana kabla ya mwaka 1931 lakini "Utaridi" ni jina linalopatikana tangu zamani kwa Kiswahili likimaanisha sayari ya kwanza.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes