Rapa aliyekuwa kwenye kundi la G Unit kabla halijasambaratika amehukumiwa kwenda jela miezi saba.
Young Buck ’35’ jumatano hii amekiri mbele ya mahakama kuvunja masharti ya kifungo cha nje chini ya uangalizi wa polisi na kuhukumiwa kurudi jela miezi saba.
Kupitia Instagram Buck aliomba marafiki zake wawe karibu na yeye akiwa jela
Young Buck alianza kuishi maisha chini ya uangalizi wa polisi toka mwaka 2013 na hapa kati amekuwa akivunja masharti ya kifungo cha nje kwa kukutwa akiwa ametumia marijuana kwenye vipimo vya mkojo na makosa tofauti ya fujo.
Post a Comment