Latest in Tech

DRAKE AJADILIWA NA HALMASHAURI YA JIJI LA TORONTO JUU YA MPANGO WAKE WA KUSIMAMISHA BONGE LA MJENGO

Drake anajenga jumba kubwa la kifahari ambalo ukubwa wake umeufanya uongozi wa Toronto ukae chini kujadiliana iwapo aruhusiwe kuendelea na ujenzi.
13108724_727100560765504_1238839032_n
Mkutano huo utafanyika May 26 kupitia iwapo watampa ruhusa ya kuporomosha kasri lake. Mipango ya ujenzi wa nyumba hiyo ni mikubwa kuliko sheria ya Toronto inavyoruhusu.
Drake aliwasilisha mipango ya kujenga nyumba yenye ukubwa wa futi za mraba 21,000 ambako tayari ametumia zaidi ya dola milioni 6 kwenye eneo hilo lenye heka 2.
Ndani ya nyumba hiyo kutakuwa na uwanja wa kikapu, bwawa la kuogelea, jumba la sinema, jumba la makumbusho kuweka vitu vyake na vingine.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes