FA imetangaza kuipiga faini Chelsea ya pound 375,000 ambazo ni sawa Tsh bilioni 1 ya kitanzania, wakati klabu ya Tottenham Hotspurs imepigwa faini ya pound 225,000 ambayo ni zaidi ya Tsh milioni 700 za kitanzania, maamuzi yametokana na wachezaji wa timu hizo kufanyiana vitendo visivyo vya kinidhamu wakati wa mchezo dhidi yao.
Mechi hiyo ilichezwa Stamford Bridge iliisha kwa sare ya goli 2-2, lakini muamuzi alitoa jumla ya kadi za njano 12, hata hivyo mapema mwezi huu Mchezaji Mussa Dembele wa Tottenham alifungiwa mechi sita kutokana na kumpelekea vidole Diego Costa wa Chelsea machoni kwa makusudi.
Post a Comment