Mkali wa hiphop Common amepata shavu la kuigiza kwenye filamu ya 24 Hours To Live, kwa mujibu wa tovuti ya Variety.
Common anayetokea mjini Chicago ataigiza pembeni ya mwigizaji Xu Qing na Ethan Hawke. Filamu ya 24 Hours To Live inahusu muuwaji anayepewa nafasi ya mwisho ya kuishi na mwajiri wake.
Common alishinda tuzo kubwa ya Academy Award kwa wimbo bora kwenye filamu ya mwaka 2014 ya Selma, na ameigiza kwenye filamu za Barbershop: The Next Cut, filamu zingine ni pamoja na Entourage and Run All Night, Now You See Me na Pawn.
Post a Comment