Mshambuliaji wa kilabu ya Real
Madrid Cristiano Ronaldo alichechemea na kutoka nje dakika chache kabla
ya kukamilika kwa mazoezi siku ya Jumanne,na hivyobasi kuzua uvumi
kuhusu uzima wake kwa kombe la vilabu bingwa Ulaya.
Mchezaji huyo
bora aliyewahi kushinda taji la Ballon d'Or anauguza jeraha la paja
ambalo lilimlazimu kukosa mechi tatu mnamo mwezi Aprili.Real Madrid itakabiliana na Atletico Madrid mjini Milan wikendi hii katika marudio ya mechi ya fainali ya 2014 ambapo Real iliibuka mshindi.

Post a Comment