Mbunge huyo amemuomba Rais John Magufuli kuagiza wabunge wa aina hiyo
ambao hata hivyo hakuwataja wapelekwe Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili
kufundishwa nidhamu.
Msabaha ametoa kauli hiyo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia
hotuba ya bajeti ya wizara ya Ulinzi na JKT iliyowasilishwa na Waziri
mwenye dhamana na Wizara hiyo, Dk Hussein Mwinyi.
“Wabunge nao waende JKT kwa sababu hili Bunge wameingia vijana
wengine ambao ni mateja wa unga na wengine wanavuta bangi. Wengine
wanawavua mama zao nguo,” amesema Msabaha.
“Wengine mama zao wameshakufa wanakuja humu wanawatukana mpaka wazazi
wao. Kwa hiyo niombe Rais Magufuli vijana wote wabunge ambao hawana
nidhamu waende JKT,” alisisitiza.
Mbunge huyo amesema wabunge wa aina hiyo hawana viwango vya
kuzungumza ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria hivyo ni vyema
waende JKT ili wakirudi wawe wamejua namna ya kuchangia.
Ingawa hakumtaja Mbunge yeyote, lakini mchango ulioibua mtafaruku
bungeni ni wa Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyedai wabunge wa viti
maalumu Chadema huitwa Baby ili kupewa nafasi hiyo.
Tafsiri ya kauli hiyo ni kuwa wabunge wa viti maalum Chadema lazima
wafanye mapenzi au kuwa na mahusiano na viongozi wa juu wenye mamlaka
ndani ya chama hicho ndipo wateuliwe kuwa wabunge.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment