Beyonce na mumewe Jay Z wameamua kwenda kupumzika kwa muda kwa kutembelesa baadhi ya nchi za Ulaya ikiwemo Ufaransa na Italia. Wawili hao wamelazimika kusimamisha ratiba zao ikiwemo ziara ya Beyonce iliyopewa jina la ‘Formation World Tour’.
Hivi karibuni jarida la Forbes liliwatangaza Queen Bey na Jay Z ndiyo couple iliyoingiza fedha nyingi zaidi kwa mwaka jana kwa kuingiza kiasi cha dola milioni 107.5.
Mwezi uliopita mastaa hao wakiongozana na mtoto wao Blue Ivy walienda vacation kwenye kisiwa cha Hawaii na baadae wakaendelea na ratiba zao nyingine.http:
Na sasa Beyonce na Jay Z wameambatana tena na mtoto wao kwenye vacation yao kwenye bara la Ulaya na tayari wameshatembelea kwenye mnara wa Eiffel Tower uliopo nchini Ufaransa ambao kiwango cha juu cha kutembelea hapo ni Euro 1,700 na Lake Como lililopo nchini Italia.
Couple hiyo inaendelea kufurahia maisha na kujitengenezea pepo yao duniani kutokana na kuendelea kuingiza fedha nyingi huku albamu ya ‘Lemonade’ iliyotarajiwa kuwagombanisha wawili hao kuzidi kufanya vizuri sokoni.
Post a Comment