Latest in Tech

MICHEZO

SIASA

VIDEOS

Latest Updates

Showing posts with label HABARI. Show all posts
Showing posts with label HABARI. Show all posts

Programu ya kampeni za Hillary Clinton yafichuliwa

06:00:00
Maafisa wa upelelezi nchini Marekani wamesema kuwa programu ya komputa inayotumiwa na jopo linalosimamia kampeni ya Bi Hillary Clinton imedukuliwa.
Mameneja wanaosimamia kampeni ya Bi Clinton walisema kuwa wadukuzi hao wameingilia mawasiliano katika kompyuta hiyo.
Awali kamati ya jopo hilo inayosimamia ukusanyaji pesa za kampeni ilisema kuwa mawasiliano yake yalikuwa yamedukuliwa.
Vyombo vya habari Marekani vinasema kuwa udukuzi huo huenda unahusika na shughuli za upelelezi za Urusi.
Image copyrightAP
Image captionHillary Clinton
Shirika la upelelezi la Marekani la FBI nalo linasema kuwa linaendelea na uchunguzi kuona iwapo makundi mengi zaidi yanaendesha udukuzi huo dhidi ya kompyuta za chama cha Democratic.
Juma lililopita mtandao wa kufichua habari za siri wa Wikileaks, unaodhaniwa kuwa na uhusiano mkubwa na Urusi ulifichua barua pepe nyingi kuhusiana na chama cha Democratic.

Ndege asafiri kutoka Finland hadi Uganda

05:57:00
Ndege mmoja ambaye inaaminika alitoka nchini Finland amepatikana katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda.
Ndege huyo aina ya Osprey kwa sasa anatunzwa na maafisa wa kituo cha kuwahudumia wanyama cha Uganda Wildlife Education Centre (UWEC).
Image copyrightUWEC
Ndege huyo mkubwa, aina ya mwewe, aligunduliwa na maafisa wa uwanja wa ndege katika njia inayotumiwa na ndege kupaa na kutua katika uwanja wa huo wa Entebbe.
Isaac Mujaasi, afisa wa mauzo na mawasiliano katika UWEC, ameambia BBC kwamba ndege huyo alikuwa ameumia katika mabawa yake baada ya kugongwa na ndege iliyokuwa inapaa.
Image copyrightUWEC
Alikuwa na pete yenye maelezo kumhusu mguuni ambayo inaashiria kwamba alimilikiwa na makumbusho ya historia asilia nchini Finland.
Bw Mujaasi anasema waliwasiliana na maafisa wa makumbusho hao ambao wamethibitisha kwamba ndege huyo ni wao.
Image copyrightUWEC
“Hili lilituthibitishia kwamba ndege huyu alisafiri kutoka Helsinki, Finland,” Bw Mujaasi amesema. “Tutamtibu ndege huyo na akipona tutamwachilia na huenda akarejea kwao.”
Afisa huyo hata hivyo amesema ni kawaida kwa ndege kuhama kutoka Ulaya, hasa wakati wa majira ya baridi na kukimbilia maeneo yenye joto.
Image copyrightUWEC

Wanasayansi wagundua dawa kwenye pua ya mwanadamu

03:51:00
Wanasayansi nchini Ujerumani wanasema wamegundua kwamba kuna chembechembe hai kwenye pua ya mwanadamu ambayo inaweza kutumia kuua viini hatari.
Dawa nyingi za kuua viini vinavyosababisha maradhi hutolewa kutoka kwenye wanaoishi kwenye mchanga.
Lakini kutokana na hali kwamba viini vinavyosababisha magonjwa mengi vimeanza kuwa sugu na kutosikia dawa, wanasayansi wamekuwa wakitafuta njia nyingine za kupata dawa mpya.
Ripoti ya vipimo imebaini katika jarida la asili kwamba dawa aina ya Lugdunin, inaweza kutibu maambukizi ya maradhi yasiyosikia dawa.
Watafiti katika chuo kikuu cha Tubingen nchini Ujerumani, waliogundua chembe hizo wanasema kuwa mwili wa binaadamu ni chanzo cha dawa mpya ambazo bado hazijatumiwa.
Dawa ya mwisho kugunduliwa katika mwili wa binadamu ilipatikana mwaka 1980.

Mbunge ajitoa mhanga Somalia

06:30:00
Watu takriban 13 waliuawa kwenye shambulio hilo
Mmoja wa washambuliaji wa kujitoa mhanga waliohusika katika shambulio lililotekelezwa karibu na kambi ya vikosi vya Umoja wa Afrika (AU) mjini Mogadishu mnamo Jumanne aliwahi kuwa mbunge.
Salah Nuh Ismail, 57, alikuwa miongoni mwa watu 13 waliofariki kwenye milipuko miwili iliyotokea karibu na uwanja wa ndege, kundi la al-Shabab lilisema.
Alijulikana sana kama Badbado, jina ambalo maana yake ni ‘Usalama’ au ‘Yule Salama’.
Alijiunga na Bunge la Somalia mwaka 2000 lakini akajiuzulu na kujiunga na al-Shabab mwaka 2010.
Anakumbukwa sana kwa kuwaita wabunge wenzake “makafiri”, baada yake kujiunga na kundi hilo la Kiislamu.
Alipokelewa kwa heshima kubwa na maafisa wakuu wa kundi hilo ambao walisema “alijutia makosa aliyokuwa ameyatenda”.
WashambuliajiImage copyrightBB
Image captionWashambuliaji wawili wa kujitoa mhanga walihusika
Tofauti na washambuliaji wengine wa kujitoa mhanga, ambao huwa vijana na watu wasiosoma sana na ambao si maarufu, yeye alikuwa mtu mzee kwa umri, aliyeelimika na mtu maarufu.
Al-Shabab wamekuwa wakikabiliana na serikali ya Somalia ambayo huungwa mkono na Umoja wa Afrika na jamii ya kimataifa.
Eneo la karibu na uwanja wa Mogadishu hulindwa sana na hutumiwa kwa shughuli za Umoja wa Mataifa.
Mataifa mengi yana afisi za kibalozi eneo hilo.

Kutizama Tv kunaweza kukuua, utafiti

06:28:00
Kutizama televisheni kwa muda mrefu ni hatari kwa maisha yako
Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Japan umethibitisha kwamba kukaa kwa mda mrefu na kutazama vipindi vya televisheni kwa masaa mengi kunahatarisha afya kwani huhusishwa na maradhi yanasababisha mzunguko wa damu mwilini kutokuwa sawa.
Watafiti hao wanasema, hali hiyo pia huenda ikasababisha damu kuganda na kutengeneza vidonge katika sehemu kama vile miguu, na iwapo mgando huo utasukumwa na nguvu za mzunguko wa damu na kuingia sehemu kama vile mapafu, husababisha vifo.
Utafiti huo ulihusiha watu zaidi ya 86,000 ambao hupendelea kutazama televisheni katika mida mbalimbali kwa siku.
Kisha afya zao zilifuatiliwa kwa zaidi ya miaka 19 tangu mwaka 1988 hadi 1990.
Matokeo yalikuwa kila muda wa masaa mawili yalipopita mtu akikaa kutazama televisheni, nayo hatari ya kupata ugonjwa huo wa mapafu uitwao ‘Fatal pulmonary embolism’ ulioongezeka kwa asilimia 40%.
Image copyrightTHINKSTOCK
Image captionWaliotazama vipindi vya televisheni kwa zaidi ya saa 5 walikuwa katika hatari zaidi kuliko waliotazama televisheni kwa mda wa chini ya saa 3.
Iligundulika pia kuwa waliotazama vipindi vya televisheni kwa zaidi ya saa 5 walikuwa katika hatari zaidi kuliko waliotazama televisheni kwa mda wa chini ya saa 3.
Zaidi ya hayo watu huambatanisha kitendo cha kukaa na kutazama televisheni huku wakila vitafunio kama vile Popcorns na Crisps ambavyo pia huwasababishia si tu mwili kukosa mazoezi bali pia kuongezeka kwa uzito unaohatarisha afya.

Wavulana wavalia sketi shuleni Uingereza

05:22:00
Wavulana wanne katika shule moja nchini Uingereza wamefika shuleni wakiwa wamevalia sketi kulalamikia hatua ya mwalimu kuwaadhibu kwa kuvalia kaptura siku yenye joto kali zaidi nchini humo.
Wanafunzi hao wa darasa la mwaka wa tisa katika shule yaLonghill eneo la Rottingdean, Sussex Mashariki, walikuwa miongoni mwa wanafunzi 20 wavulana waliovalia kaptura za kuvaliwa wakati wa mazoezi badala ya suruali ndefu.
Baadhi walifukuzwa shuleni Jumanne na wengine kutengwa hadi siku iliyofuata. Waliokubali kuvua kaptura hizo na kuvalia suruali ndefu hawakuadhibiwa.
Lakini badala ya kuvalia sare kamili ya wakati wa masomo, kama walivyokuwa wameagizwa, wanafunzi wanne walirejea shuleni Alhamisi wakiwa wamevalia sketi.
ParkerImage copyrightANGELA PARKER
Image captionMichael Parker, mmoja wa wanafunzi, akiwa na kaptura na akiwa na sketi
Watatu waliambia wavue sketi hizo lakini wote kwa pamoja wakakataa na ndipo wakaruhusiwa kuendelea kukaa shuleni.
Mwalimu mkuu Kate Williams aliwaambia wanaweza kuvalia mavazi yoyote, mradi yawe ni sehemu ya sare iliyokubalika shuleni.

Watu 20 wauwa kwenye mlipuko nchini Afghanistan

06:13:00
Wizara ya afya ya Afghanistan imesema takriban watu ishirini wameuawa na zaidi ya wengine 150 wamejeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga lililofanyika kwenye mji mkuu Kabul.
Baadhi ya taarifa zinasema kulikuwa na milipuko miwili.
Shambulio hilo linaonyesha kuwa lililenga maandamano ya maelfu ya watu kutoka jamii ndogo ya Hazara, ambao hujikuta wakidhalilishwa na kufanyiwa ukatili.
Walikuwa wakiandamana kupinga mpango wa serikali wa kuhamisha umeme kutoka kwenye majimbo yao katikati ya nchi.

Analipwa kubikiri watoto ili kuondoa mikosi Malawi

06:49:00
Katika tamaduni nyingi kote duniani mwanamke anapoolewa huwa ni fahari kubwa sana akiwa ni bikira.
Mathalan ni dhihirisho la mwanamke kuwa amelelewa na kutunzwa vyema.
Ni dhihirisho la usafi.
Hata hivyo jamii moja nchini Malawi haithamini ubikira wa watoto wao wa kike.
Amini usiamini wazazi huwa wanamlipa ''Fisi'' kumbikiri binti yao punde tu anapopata hedhi yake ya kwanza.
Image captionAniva huchemsha mizizi hiyo kabla ya kuanza kubikiri watoto kwa takriban siku 3 hivi
Wanaamini kuwa binti ambaye ni bikira ni mkosi kwa jamii!
Malimwengu haya.
Wazazi na jamii kwa jumla katika maeneo mengi ya kusini mwa Malawi wamekuwa wakishikilia tamaduni hii kwa miaka na mikaka.
''Fisi'' ama wanaume wanaowabikiri watoto wa kike huchaguliwa na wazazi kuwaondolea mikosi.
 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes