![]() |
Trump na Senecal |
Huduma ya ujasusi ya Marekani
imeanzisha uchunguzi baada ya aliyekuwa muhudumu mkuu wa nyumbani kwa
Donald Trump kutaka rais Barrack Obama auawe.
Bwana Senecal alimfanyia kazi bwana Trump,mgombea wa urais kupitia chama cha Republican kwa takriban miaka 30.
Kampeni ya Trump hatahivyo ilijiepusha na matamshi ya Senecal.
''Hakuajiriwa na Trump na hajaajiriwa tangu mwezi Juni 2009'', alisema msemaji wa kampeni ya Trump Hope Hicks katika taarifa.

Na baadaye siku ya Alhamisi, bwana Senecal mwenye umri wa miaka 84 alikiambia chombo cha habari cha CNN kwamba Obama anafaa kunyongwa nje ya Ikulu ya White House.
Pia aliitaja Ikulu ya White House kuwa ''msikiti mweupe''.
Post a Comment