Klabu ya Norwich City imeshushwa daraja kutoka Ligi ya Premia licha ya kuandikisha ushindi dhidi ya Watford.
Ushindi wa Sunderland wa 3-0 dhidi ya Everton Jumanne uliwafikisha hadi alama 38 na kwa kuwa Norwich na Newcastle hawawezi kuwafikia, moja kwa moja klabu hizo mbili zikashushwa daraja.

Troy Deeney alikuwa amewapa Watford uongozi mechi hiyo iliyochezewa Carrow Road lakini Norwich wakajibu kupitia bao la Nathan Redmond.
Dieumerci Mbokani aliwafungia Norwich la pili naye Craig Cathcart akawaongezea la tatu kwa kujifunga.
Odion Ighalo alikomboa bao la pili lakini Mbokani akawafungia Norwich bao la nne.
Baada ya kushushwa daraja, Norwich sasa watakuwa wakichezea tu fahari mechi yao ya mwisho dhidi ya Everton Jumapili.
Watford watajaribu kumaliza msimu vyema dhidi ya Sunderland nyumbani
Post a Comment