Mrembo anayetikisa kwa sasa kwenye kizazi cha mitindo Bongo, Hamisa Hassan Mobeto, anadaiwa kutaka kumuua kwa presha mzazi mwenzake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’, kufuatia kuvuja kwa habari kwamba, amejibinafsisha penzi la nyota huyo, Amani limechimba.
Chanzo cha habari kimenyetisha kwa Amani hivi karibuni kwa kusema kwamba, nyumbani kwa Diamond, Madale jijini Dar hakuna amani hata kidogo kufuatia mtifuano mkali baina ya Zari na wifi yake (Esma) na mkwe wake (Sanura Kasim) ambapo kisa chote kinadaiwa kusababishwa na Mobeto ambapo wengi wanasema ni mpenzi mpya wa Diamond kwa sasa na kwamba, ndugu ndiyo wanamkubali kuliko ‘Mzungu’ Zari.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment