Latest in Tech

Hiki ndicho kiasi cha Pesa alichokuwa akilipwa Hanscana na Wanene Entertainment.

Kama ulikuwa una shauku ya kujua kiasi cha pesa ambacho muongozaji wa video nchini Hanscana alikuwa analipwa na studio za Wanene,uongozi wa studio hizo wametaja kiasi walichokuwa wakimlipa director Hanscana.
Akiongea kwenye kipindi cha funiko base,Gentriez ambaye ni mmoja watu wa ndani wa kampuni hiyo amesema Hascana alikuwa analipwa sjilingi milioni mbili kila mwezi na studio hizo na pia video zote alizokuwa akizifanya pesa zilikuwa zinaingia kwa Hanscana.
Wanene tulikuwa tunamlipa mshahara hata kabla kampuni haijafunguliwa tulikuwa tunamlipa na video alizokuwa akifanya pesa yote ilikuwa inaingia mfuko kwa Hascana kwa hiyo wanene walikuwa wamewekeza kwake lakini baada ya kufungua kampuni ilibidi kwenye kila kazi lazima kuwe na percent ya kampuni..tulikuwa tunamlipa milioni mbili kwa mwezi” alifunguka Gentriez

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © bakinamimi. Designed by OddThemes & VineThemes